Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinapenda kuwataarifu waombaji kazi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 10, 11, 12 na 13 Machi, 2025 kuwa, majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Aidha ajira zao zitakuwa rasmi pale vyeti vyao vitakapohakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika.
Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za ajira kwa kufika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuanzia tarehe 28 Machi, 2025 saa tatu kamili asubuhi, wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili ili zihakikiwe kabla ya kupewa barua za ajira.
Leave a Comment