Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Medical Centre anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote waliomba kazi kuwa, usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 29 Julai, 2025 hadi 01 Agosti, 2025. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelezo yafuatayo: –
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyoonyeshwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu ambapo usahili utafanyika umeanishwa kwa kila Kada.
2. Usaili wa mchujo kwa Kada utafanyika kuanzia tarehe 29 hadi 31 Julai, 2025.
3. Wasailiwa watakao faulu usaili wa mchujo, watafanya usaili wa kuongea kadri ya maelekezo.
4. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi
5. Vitambulisho vitakavyokubalika ni pamoja na:- Kiambulisho cha mkazi, Kitambulisho cha mpiga kura, kitambulisho cha kazi, kitambulisho cha Taifa au Hati ya kusafiria.
6. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI NA “TRANSCRIPT”, kuanzia cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha Nne, Sita, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya juu, Shahada na kuendelea kutegemea na sifa za mwombaji.
7. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provision Results, Statement of Results, Hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita, (Form Four and Six Result slips). HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
8. Kila msailiwa atajighramia kwa chakula, usafiri na malazi.
9. Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
Leave a Comment