Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Majina ya Walimu Walioitwa Mafunzo ya Somo la Elimu ya Biashara 2025

Majina ya Walimu Walioitwa Mafunzo ya Somo la Elimu ya Biashara 2025

YAH: RUHUSA YA WALIMU WA AJIRA MPYA WANAOFUNDISHA SOMO LA ELIMU YA BIASHARA KIDATO CHA I – IV KUHUDHURIA MAFUNZO YA SIKU TATU (3)

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Shirika la Educate! inatarajia kutoa mafunzo kwa walimu wa ajira mpya na kuripoti katika vituo vyao vya kazi mpaka sasa wapatao 1,571 kufundisha Somo la Elimu ya Biashara, yaani Business Studies kwa shule za sekondari za serikali Tanzania Bara. Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea walimu uwezo wa kutumia mbinu mbalimbali za kufundishia Somo la Elimu ya Biashara kwa wanafunzi wa kidato cha I – IV. Mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu tatu kuanzia tarehe 27/05-11/06/2025 katika vituo tofauti kwa muda wa siku 3 kama inavyoonekana kwenye jedwali ambatishwa. Pia, mafunzo yatakuwa ni “residential” ambapo walimu watalala katika kituo husika cha Mafunzo ili kuwezesha ratiba kutekelezwa kwa ufanisi. Aidha, mafunzo yatatanguliwa na uzinduzi maalumu utakaofanyika tarehe 27 Mei, 2025 katika chuo cha Ualimu Tabora kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Walimu waliopangwa kuhudhuria mafunzo katika kituo hiki wanapaswa kushiriki katika uzinduzi huo katika tarehe tajwa.

Ninaandika barua kukuomba kuwaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa kuwaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaruhusu walimu (Rejea orodha iliyowasilishwa TET kutoka TAMISEMI) kuhudhuria mafunzo katika vituo vilivyooneshwa kwenye jedwali ambatishwa kwa kuzingatia tarehe pendekezwa. Walimu waelekezwe pia kuja na vifaa vya kujifunzia kama vile kompyuta mpakato, vishikwambi, na simu janja ili utekelezaji wa mafunzo uwe na ufanisi. Aidha, Walimu wanaelekezwa kubeba chandarua, taulo na
shuka/blanketi kwa ajili ya matumizi yake binafsi wakati wote wa mafunzo akiwa katika
kituo cha Mafunzo.

Walimu watapatiwa posho maalumu ya shilingi 60,000/= kwa siku ambayo itakuwa kwa ajili ya kugharamia mahitaji yao ikiwemo malazi yao binafsi katika hosteli za chuo husika. Pia, serikali itatoa nauli na huduma ya chakula kwa walimu katika siku zote za mafunzo. Ratiba ya mafunzo itaanza saa 2:00 asubuhi na kuhitimishwa saa 12: 00 jioni katika siku zote za mafunzo. Pamoja na Barua hii, majina ya walimu yameambatishwa ili kuwawezesha wakurugenzi kurejelea majina ya walimu husika.

PAKUA PDF HAPA

Leave a Comment