Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TARURA Manyara, February 2025

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TARURA Manyara, February 2025

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245 na kutangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Na. 211 la tarehe 12 Mei 2017. Wakala ulianza kufanya kazi rasmi tarehe 1 Julai 2017 na sasa Wakala umefikisha takribani miaka 5 toka kuanzishwa kwake.

Lengo Kuu la Uanzishwaji wa TARURAni kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati jukumu la Menejimenti ya Mtandao wa Barabara za Wilaya lilipokuwachini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa(MSM) 184, lakini vilevile pamoja na kukabiliana na mabadiliko katika sekta ya barabara kwa nia ya kuboresha huduma na kuongeza ufanisi.

Jukumu kubwa la TARURA ni kusimamia matengenezo, ukarabati na ujenzi wa Mtandao wa Barabara za Wilaya wenye jumla ya Kilomita 144,429.77 zilizokuwa zikisimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa 184 na kuratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI chini ya Idara ya Miundombinu.

Kwa niaba ya Mtendaji Mkuu, Meneja wa TARURA Mkoa wa Manyara anayofuraha kuwaalika wote walioteuliwa kuhudhuria usaili wa nafasi ya kazi (Udereva), utakaofanyika Februari 24,2025 hadi Februari 26, 2025 kuanzia saa 8:00 Asubuhi katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria – Manyara.

PAKUA PDF HAPA CHINI

CALL FOR INTERVIEW MANYARA REGION

Leave a Comment