Orodha ya Maswali ya Usaili Ajira Mpya za Walimu, haya ni maswali ya yanayoulizwa katika usaili wa walimu somo lolote katika interviews zote za utumishi PSRS. Maswali haya yanagusa Education Management, Psychology, Philosophy, Theories na Content kwa Ujumla katika baadhi ya masomo.
Mwaka huu serikali imeanza kufanya usaili wa kada za ualimu tofauti na utaratibu wa zamani. Usaili huo unaendeshwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (Utumishi), Ofisi ya Rais-Tamisemi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Afya, Tume ya Utumishi wa Walimu, ofisi za wakuu wa mikoa yote na wataalamu kutoka katika taasisi za umma.
Kikawaida mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma huendeshwa na Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya mamlaka za ajira katika Utumishi wa Umma zinazojumuisha: Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali; Mamlaka za Serikali za Mitaa; Taasisi na Mashirika ya Umma.
Sheria iliyoanzisha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeweka bayana mipaka ya majukumu ambapo, ajira zote zinazohusu: Mhimili wa Bunge; Mhimili wa Mahakama; na vyombo vya ulinzi na usalama zinaendelea kusimamiwa na mihimili na taasisi hizo na hivyo kutoihusisha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
PAKUA PDF HAPA CHINI
Leave a Comment