Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria namba 14 ya Jeshi la Zimamoto na uokoaji ya mwaka 2007 pamoja na kanuni zake za mwaka 2008, 2012, 2014 na 2015.
Majukumu hayo ni:
- Kuzima moto
- Uokoaji
- Ukaguzi wa kinga na tahadhari za moto
- Kukusanya maduhuli ya serikali kutokana na ada ya ukaguzi wa kinga na tahadhari za moto
- Kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama wa moto n.k
MOTO NI NINI?
Moto ni muunganiko wa kikemikali kati ya joto, hewa ya oksijeni na kitu chenye uwezo wa kuungua.
Muunganiko huo unaunda pembetatu ya moto.

MOTO UNASABABISHWA NA NINI?
- Kwa asilimia kubwa moto unasababishwa na shughuli za kila siku za binadamu, na kwa kiasi kidogo na majanga ya
- Baadhi ya sababu za matukio ya moto ni:
- Uzembe/ kujisaau
- Ujinga
- Hujuma
- Hitilafu za umeme
- Ajali za barabarani
- Radi
- Milipuko
- Volkano
ili kuzuia moto ni vyema kuwa makini na shughuli zetu za kila siku.
TAHADHARI ZA KUCHUKUA ILI KUZUIA AU KUPUNGUZA MAJANGA YA MOTO
- Ili kuzuia moto usitokee inatakiwa kuzuia vitu vinavyounda pembetatu ya moto visikutane pamoja ama vikutane katika kiwango ambacho moto hauwezi kutokea.
- Mambo yafuatayo yanaweza kufanyika ili kuzuia moto usitokee:
- Vitu vinavyoweza kushika moto na kuungua viwekwe mbali na vyanzo vya moto mfano mafuta, gesi, magodoro, masofa, mafaili, vitabu, makabati, nguo n.k
- Vyanzo vya moto viwekwe mbali na vitu vinavyoweza kuungua mfano majiko, soketi/swichi,
- Watoto wasiruhusiwe kuchezea vitu vinavyoweza kusababisha moto mfano vibiriti, mafuta ya taa, vifaa vya umeme, majiko n.k
- Vyanzo vya moto visivyo vya lazima/ visivyotumika viondolewe/ visimwe.
- Usiache kitu kinachozalisha moto ndani ikiwa wewe haupo mfano jiko, pasi, heater n.k
- Vuta sigara katika mazingira salama. Usitupe ovyo vipisi vya sigara; zima na kuweka kwenye ashtray.
- Funga mifumo ya kinga na tahadhari ya moto ofisini/nyumbani.
- Weka vifaa vya kuzimia moto vya awali ofisini/nyumbani na hakikisha unajua kuvitumia mafano mitungi ya kuzimia moto, blanketi za kuzimia moto, mchanga mkavu n.k
- Pata elimu ya usalama wa moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
- Fanyiwa ukaguzi wa kinga na tahadhari za moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ofisini/nyumbani.
Nunua na tumia vifaa original vya umeme.
- Tumia wataalamu kutengeneza vifaa vya umeme au kufanya ufundi wowote kuhusu umeme.
- Zima vifaa vya umeme na chomoa cable kama havina matumizi.
- Ikiwa umeme unazimikazimika pasipo na sababu ya msingi wasiliana na wataalamu (TANESCO).
- Toa taarifa ya moto mapema zimamoto kwa namba ya simu 114
KWANINI MOTO NI HATARI?
- Moto ni hatari kwa sababu:
- Unasababisha vifo na matatizo ya kiafya kutokana na moshi au joto kali.
- Unateketeza mali na kuleta hasara kubwa.
- Vitu vilivyoungua havitengenezeki.
- Unazuia shughuli za kijamii kuendelea
- Moto unazalisha hewa za sumu zinazosababisha kifo mfano CO, HCN, HCL, SO₂ n.k
- Moshi unasababisha kutoona vizuri katika mazingira ya moto.
MBINU ZA UZIMAJI MOTO
- Ili moto uweze kuzimika kwa urahisi unatakiwa kuuwahi ukiwa katika hatua za awali kabla haujawa mkubwa.
- Moto una hatua 5 za ukuaji
- Uwakaji/ignition
- Ukuaji/growth
- Usambaaji/flashover
- Moto mkubwa/ full developed
- Uzimikaji/ decay
- Moto unaweza kuzimika kwa urahisi ukiwa katika hatua za uwakaji au ukuaji.
- Hatua zilizobaki moto unakuwa umeshakuwa mkubwa uwezekano wa kuzimika unakuwa mdogo.
- Moto unaweza kuzimwa kwa njia tatu ambazo ni upoozaji/cooling, uondoaji wa hewa ya oksijeni/smothering na uondoaji wa kitu kinachoungua/starvation.
- Tunatumia maji kufanya upoozaji
- Ili kuondoa hewa ya oksijeni katika moto tunatumia mchanga mkavu, dry powder, blanketi, carbon dioxide na fomu.
- Ili kuondoa kitu kinachoungua tunatumia kifaa chochote kisichoweza kushika moto kwa urahisi.
- Mbinu ipi itumike wakati gani inategemea daraja la moto husika.
- Usifanye kitu kwa kubahatisha. Fanya kitu sahihi kwa wakati sahihi ili kuepusha madhara yasiyo ya lazima.
MADARAJA YA MOTO
Kuna madaraja makuu manne ya moto:
- Daraja A – moto wa vitu vya kawaida. Tunatumia maji kuzima moto daraja A.
- Daraja B – moto wa vimiminika/mafuta. Hatutumii maji. Tunatumia fomu kuzima moto daraja B. pia unaweza kutumia carbon dioxide, dry powder, mchanga mkavu, balnketi.
- Daraja C – moto wa gesi. Hatutumii maji. Tunatumia carbon dioxide kuzima moto daraja C. pia unaweza kutumia mchanga mkavu au dry powder.
- Daraja D – moto wa metali/ vitu vyenye asili ya chuma. Hatutumii maji. Tunatumia dry powder, pia haishauriwi kutumia carbon dioxide.
NB:
- DRY POWDER ina uwezo wa kuzima madaraja yote ya moto.
- Kama unatumia maji kuzima moto sehemu yenye umeme, zima umeme kwanza.
- Tumia kizimia moto sahihi kwa daraja husika la moto.
Leave a Comment