MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA UFUNDI STADI KWA MSIMU WA DESEMBA, 2024
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuufahamisha umma kuwa limeidhinisha matokeo ya Mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi katika ngazi ya I, II na III iliyofanyika mwezi Desemba, 2024. Mitihani hiyo iliratibiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Jumla ya watahiniwa 41,331 walifanya mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi ambapo wasichana ni 14,215 sawa na asilimia 34.4 na wavulana 27,116 sawa na asilimia 65.6.
Matokeo ya Mitihani
Kati ya watahiniwa 41,331 waliofanya mitihani, watahiniwa 35,355 sawa na asilimia 86 wamefaulu. Watahiniwa 5,976 sawa na asilimia 14 wanapaswa kurudia mitihani yao.
Matokeo ya mitihani hiyo ni katika fani za Ufundi Magari, Ufundi Umeme, Ushonaji, Uchapaji, Usindikaji Vyakula, Huduma za Biashara, Kilimo, Madini, Ukarimu na Utalii pamoja na Urembo.
Kufutiwa matokeo
Watahiniwa wawili (2) wamefutiwa matokeo yao kutokana na ukiukwaji wa taratibu za mitihani.
Kupata matokeo ya mitihani ya CBA, Uanagenzi na NABE kwa msimu wa Desemba, 2024 bonyeza hapa Chini
| TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA UFUNDI STADI MSIMU WA DESEMBA 2024 |
|---|
Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe: dac@veta.go.tz na namba ya simu 0755267489
Leave a Comment