Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Saba (PSLE) 2025/2026 imetoka unaweza kupakua na kuisoma HAPA.
MAELEKEZO MUHIMU
1.Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Mtihani ya mwaka 2025 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani
la Tanzania.
2. Hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kuthibitisha kuwa somo
hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Mtihani.
3. Kabla ya kufungua bahasha, mpe Mtahiniwa asome kwa sauti jina la somo lililoandikwa juu ya
bahasha ili kuthibitisha ni somo husika kwa mujibu wa ratiba.
4. Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo katika Karatasi ya Mtihani na Ratiba
ya Mtihani, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya Mtihani husika ndiyo yatakayofuatwa.
5. Watahiniwa wenye mahitaji Maalum (Wasioona, Uoni hafifu, Viziwi) waongezewe MUDA WA
ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa somo la Hisabati na DAKIKA 10 KWA KILA
SAA kwa masomo mengine.
6. Watahiniwa wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za Mtihani zenye maandishi
yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
7. Watahiniwa waelekezwe;
(a) Kuingia ndani ya chumba cha Mtihani nusu saa kabla ya muda wa Mtihani na
watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya Mtihani kuanza hawataruhusiwa.
(b) Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa Mtihani.
(c) Kuandika namba ya Mtihani kwa usahihi.
(d) Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina yao. Ikiwa Mtahiniwa ana
tatizo anatakiwa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa Mtihani.
(e) Kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani kwani watakaojihusisha
matokeo yao yatafutwa.
Matokeo ya Mock Darasa la Saba Mikoa Yote Tanzania 2025
Shule za msingi Tanzania zimetangaza matokeo ya darasa la saba kwa mitihani ya mock iliofanyika katika shule mbalimbali za msingi ili kupima uwezo na ufaulu wa wanafunzi kuelekea mtihani wa mwisho wa darasa la saba itakayo fanyika mwezi wa Tisa 2025
Matokeo ya mock kwa darasa la saba unaweza kuyapata kupitia tovuti ya mkoa husika au kwenda shuleni kupata matoke hayo au kuwasiliana na shule husika ili kukupatia matokeo ya mwanafunzi.
Leave a Comment