SHULE YA MSINGI S.L.P 1…………,
TAREHE ………………………….
MWL. ………………………………………………………………..
SHULE YA MSINGI
YAH:KUTEULIWA KUWA MWALIMU WA CHAKULA NA AFYA SHULENI.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, kufuatia taratibu na kanuni za kazi katika utumishi wa Umma zinavyoelekeza. Kwa mamlaka niliyonayo kama Mwalimu mkuu Napenda kukutaarifu kuwa nimekuteua kushika nafasi tajwa hapo juu hadi hapo nitakapoamua kukubadilisha katika nafasi hiyo. Kama mwalimu wa afya na lishe una wajibu wa kusimamia yafuatayo:
i.kuhakikisha unaunda klabu mbalimbali kama vile klabu ya afya na usafi.
ii.kuhamasisha uboreshaji wa usafi na afya pamoja na usafi binafsi kwa wanafunzi shuleni.
iii.kutengeneza muundo wa uongozi katika kila klabu.
iv.kuandaa mpango wa utekelezaji wa shughuli za klabu kwa muda maalumu.
v.kuhamasisha wanafunzi kujiunga na klabu ya afya na usafi shuleni.
vi.kuhamasisha na kusimamia upatikanaji na utoaji wa chakula shuleni.
vii.kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama,viwanja vya michezo,vyoo na uimarishaji wa haki za mtoto shuleni.
viii.kumshauri mwalimu mkuu kuhusu mambo yote yahusuyo afya na usafi wa wanafunzi shuleni.
ix.kufanya kazi zingine zote utakazopangiwa na mwalimu mkuu.
Ikitokea changamoto yeyote katika kutekeleza majukumu hayo tafadhali shirikisha Uongozi wa shule pale inapobidi kufanya hivyo.
Nakutakia utekelezaji mwema na wenye mafanikio.
Wako katika utumishi.
………………………………
Leave a Comment