Barua rasmi ni barua zinazohusu mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za barua rasmi ni kutoa taarifa, kuomba kazi au huduma, kuagiza vitu na kutoa mwaliko kwa mfano kwa kiongozi fulani wa nchi, kutoa malalamiko na kuweka kumbukumbu au marejeo.
Muundo wa Barua Rasmi
Barua rasmi au barua ya kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Kwa kawaida huwa na sehemu zifuatazo:
- Anwani ya mwaandishi –huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa karatasi.
- Tarehe ya barua hiyo– tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi
- Anuwani ya mpokeaji– Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa karatasi, na huwekwa msitari mmoja chini ya tarehe.
- Salamu– Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua rasmi au kumwuliza hali yake.Ndugu Bwana Meshaki, => taja jina lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia. Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji wa barua, tumia bw/bi
- Mada– Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama vile YAH:(yahusu). Ni sharti kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.
- Utangulizi– Hukaa chini kidogo ya mada ya barua. Haya ni maelezo mafupi yasiyozidi aya moja ambayo huelezea kusudi kuu la barua kama kidokezo.
- Ujumbe– Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.
- Tamati– mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile: Wako mwaminifu, [jina], Sahihi
PAKUA PDF HAPA CHINI
Leave a Comment