Mwalimu Daraja la IIIB huyu ni mwalimu mwenye Stashahada (Diploma ya Ualimu).
SIFA
Awe na cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu miaka mitatu (3) kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
viii. Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali anaanzia TGTS – C.
Leave a Comment