Mwalimu Daraja la IIIC huyu ni mwalimu mwenye elimu ya kuanzia Shahada (Degree).
SIFA
Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia; iii. Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule; na
viii. Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali anaanzia TGTS – D.
Leave a Comment