TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi wa shule ya Awali na Msingi ya Green Point anapenda kukutangazia nafasi za kazi ya ualimu kama ifuatavyo:
1.0 Mwalimu wa Masomo ya Sayansi – Nafasi 2
1.1 Mwalimu wa shule ya Awali(Montessori) – Nafasi 1
2.0 SIFA ZA MWOMBAJI
i. Awe raia wa Tanzania
ii. Awe Mwadilifu na hajawai kushtakiwa kwa makosa ya jinai.
iii. Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya kingereza vizuri.
iv. Awe tayari kuishi katika mazingira karibu na shule.
v. Awe na stashahada au shahada ya ualimu kutoka chuo cha ualimu kinachotambulika na Serekali.
vi. Awe na uwezo na uzoefu wa kufundisha kuanzia mwaka mmoja au zaidi.
vi. Mwalimu wa Sayansi awe na uwezo wa kufundisha kuanzia darasa la nne na kuendelea.
Maombi yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma,Nida/cheti cha kuzaliwa pamoja na cv ya mwombaji.
Maombi yote yatumwe kwa meneja wa shule kwa njia ya barua pepe kilalajunior@gmail.com au Whatsup kwa namba 0717345574
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 3.04.2025

Leave a Comment