Kampuni ya ASAS inayo jishughulisha na shughuli za uzalishaji wa maziwa, vinywaji baridi pamoja na shughuli za usafirishaji, inapenda kuwatangazia vijana wa kitanzania kuwa tunatarajia kuzindua kiwanda chetu kipya cha kusindika maziwa katika eneo la Chang’ombe viwandani jijini Dar es salaam, ambapo tayari tumesha fikia hatua za mwisho za uandaaji wa kiwanda hiki na kinacho subiriwa kwa sasa ni uzinduzi, kisha kuruhusu shughuli za uzalishaji zianze kufanyika. Kiwanda hiki kitaanza kufanya kufanya kazi mwezi April mwaka huu 2025.
Tunapenda kutangaza nafasi za kazi kwa vijana wa kitanzania kote nchini walio tayari kufanya kazi ndani ya kiwanda chetu.
NAFASI ZINAZO HITAJIKA
- Mhasibu (Nafasi 10 wanawake tu) Uwe na elimu ya uhasibu kuanzia ngazi ya cheti
- Fundi umeme wa viwandani (Nafasi 9) Uwe na elimu ya fani ya umeme angalau ngazi ya cheti, mwenye uzoefu wa kazi walau mwaka mmoja.
- Mlinzi (Nafasi 10) Uwe na uzoefu wa kazi angalau mwaka mmoja, na uwe umepitia mafunzo ya mgambo au JKT.
- Supervisor (Nafasi 8) Uwe na uzoefu wa kusimamia wengine, mwenye uwezo mzuri wa kufanya mawasiliano, elimu kuanzia ngazi ya cheti katika fani yeyote.
- Mapokezi (Nafasi 10 wanawake tu) Uwe na uzoefu wa kazi hii, mwenye elimu kuanzia ngazi ya cheti katika fani yeyote.
- Usafi (Nafasi 20) Uwe na elimu kuanzia kidato cha nne.
- Dreva (Nafasi 30) Uzoefu usio pungua mwaka mmoja, na kiwango cha leseni kuanzia Daraja D
- Watu wa kufanya shughuli zote za uzalishaji wa malighafi (Nafasi 215) Elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea. Hawa watapatiwa mafunzo katika kila kitengo, namna ya kuendesha mitambo ya uzalishaji na ufungaji wa bidhaa zetu hata kufikia hatua ya mwisho ya uzalishaji tayari kupelekwa sokoni.
SIFA ZA JUMLA ZA MWOMBAJI
- Awe mtanzania mwenye umri usio pungua miaka 18
- Awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea
Maombi yatumwe kwa Afisa mwajiri kupitia barua pepe ambayo ni vacancyasas@gmail.com au hrasascompanies@gmail.com Aambatanisha barua ya maombi ya kazi, vyeti vyako vya elimu pamoja na namba ya Nida au cheti cha kuzaliwa. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11/03/2025, watakao kidhi vigezo wataitwa kwa ajili ya usaili.

Leave a Comment