NAFASI YA KAZI – KATIBU MKUU WA JUKWAA LA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KANDA YA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR)
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanda ya Maziwa Makuu (FP-ICGLR). Nafasi hil itagombewa na wananchi kutoka nchi tatu wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, na Burundi, kwa mujibu wa maelekezo ya kikao cha TROIKA kilichofanyika tarehe 25 Oktoba, 2024.
MAJUKUMU YA KATIBU MKUU
Katibu Mkuu ataongoza Sekretarieti Kuu ya FP-ICGLR, na atakuwa na majukumu yafuatayo:
· Kusimamia masuala ya utawala, fedha, na usimamizi wa klufundi wa shughuli za Jukwaa;
· Kuratibu shughuli zote za Jukwaa kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama;
· Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi mbalimbali ndani ya Jukwaa;
· Kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi ya Bunge la FP-ICGLR na mipango ya kimkakati ya Jukwaa.
SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu: Shahada ya kwanza (Bachelor’s Degree) kutoka chuo kikuu
kinachotambulika.
Uzoefu: Uzoefu wa angalau miaka kumi (10) katika nafasi za uongozi wa juu katika
taasisi za kitaifa, kikanda au kimataifa.
Uwezo wa Uongozi: Sifa za uongozi, uadilifu, na weledi wa hali ya juu.
Jinsia: Moja kati ya wagombea watatu wanaopendekezwa ni lazima awe
mwanamke, kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wanapaswa kuwasilisha barua ya maombi, wasifu binafsi (CV), na nakala za vyeti vya elimu kwa njia ya barua pepe kupitia: cna@bunge.go.tz au
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro,
S.L.P. 941.
40490 Tambukareli,
DODOMA.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni ljumaa, Machi 14, 2025.
Leave a Comment