Halmashauri ya Mji Njombe inatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 08/05/2025 na kuukimbiza kwa siku moja na kukabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Songea tarehe 09/05/2025.
Kwa barua hii mnajulishwa kutuma maombi ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe.
Awe kijana kuanzia miaka 18 asizidi 35.
Elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
Awe na Afya na akili timamu.
Awe na nidhamu isiyotiliwa mashaka.
Awe ni mzalendo na yupo tayari kujitolea kwa ajili ya Halmashauri yake.
Sifa za mwombaji.
Watakao omba kukimbiza Mwenge watatakiwa kutuma maombi yao kwa; –
Aidha Mwombaji atatakiwa kuambatanisha picha mbili za passport size za hivi karibuni pamoja na Vyeti vya masomo na wasifu wake (CV).
Mwisho wa kupokea barua za maombi tarehe 10/04/2025.

Leave a Comment