Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Waadventista-Wasabato Kitungwa, unawatangazia watanzania wenye sifa kutuma maombi ya kazi ya ualimu kwa somo la Physics.
1. MWALIMU WA PHYSICS (Nafasi Moja)
MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa.
Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
SIFA ZA MWOMBAJI
Muhitimu wa Shahada ya ualimu kutoka vyuo vya elimu ya juu vinavyotambuliwa na
Awe na shahada isiyo ya ualimu/elimu yenye somo la Physics pamoja na stashahada ya ualimu(Post-graduate Diploma in Education) kutoka vyuo vya elimu ya ya juu vinanyo tambuliwa na Serikali.
Awe mwenye umri usiozidi miaka.
Awe raia wa
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao wa Whatsapp kupitia namba ya simu
+255 682 662 122. AU Maombi yawasilishwe Shuleni Kitungwa-Morogoro katika ofisi ya Katibu muhtasi wa Mkuu wa Shule.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10 Machi 2025 saa 10:00
USAILI
- Waombaji wote watakao pita kwenye mchujo watapigiwa simu na kupewa maelekezo ya kufika kwenye usaili.
- Usaili utafanyika tarehe 13 Machi 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi Shuleni Kitungwa –
- Waombaji wote watakaokuja kwenye usaili wafike na nakala halisi za vyeti.
Leave a Comment