TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkuu wa shule ya sekondari Kitungwa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi tatu za walimu kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili.
1. Mwalimu wa masomo ya biashara ( Book keeping and Commerce) – nafasi moja SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Biashara au Usimamizi wa
Biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration Business studies)
AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Biashara au usimamizi wa biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration na Business Studies) pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
2. Walimu wa somo la Hesabu (Basic Mathematics) – nafasi mbili (2)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Hesabu ( Mathematics)
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi
wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii.Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
1v. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
vi. Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
vii. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule;
viii. Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule
MASHARTI YA JUMLA.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 40
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
iii. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita, Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates
v. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
vi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 03 Julai, 2025.
vii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa Pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
HEADMASTER,
KITUNGWA ADVENTIST SECONDARY SCHOOL,
P.O. BOX 1816,
MOROGORO.
viii. Maombi yote yatumwe kwa whatsapp; +255 755 296 848 (Mkuu wa shule) au +255 682 662 122 (Makamu Mkuu wa shule) au kwa barua pepe; info@kass.ac.tz
Limetolewa na;
MKUU WA SHULE YA SEKONDARI KITUNGWA
Leave a Comment