Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Nafasi za Kazi za Mkataba Halmashauri Singida 2025

Nafasi za Kazi za Mkataba Halmashauri Singida 2025

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MKATABA.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Singida anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, katika kama (Vituo vya Afya ), Kuomba nafasi ya kazi ya mkataba wa Mwaka mmoja ifuatavyo;

1.0 KAZI YA MSAIDIZI WA HESABU DARAJA II NAFASI 02.

1.1 SIFA ZA MUOMBAJI.
. Kuajiriwa wenye cheti cha Astashahada ya uhasibu kutoka chuo kinachotambulika na Serikali au cheti cha ATEC 1 kilichotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

1.2 KAZI / MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II

· Kuandika na kutunza kumbukumbu zinazohusu shughuli za uhasibu
· Kutunza kumbukumbu za hesabu
· Kupeleka barua / nyaraka za uhasibu Benki
· Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi

1.3 MSHAHARA.

Ngazi ya Mshahara ni TGS B

2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

Waombaji wanatakiwa wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia Miaka 18 hadi 45

Waombaji wote waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa

Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wawili.

Maombi yote yaambatane na picha 1 ( Passport Size ) , Nakala za Vyeti Taaluma Vyeti vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu Mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa zilizoelekezwa hapo juu.

Waombaji wote waambatanishe Nakala za Kitambulisho cha Taifa ( NIDA) kwa ambao hawana Vitambulisho hivyo , Namba za NIDA ziandikwe kwenye maelezo binafsi ( CV ).

Testimonials “Provisional Results”, “Statement of Results”, hati matokeo ya Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) havitakubaliwa.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU NA NECTA).

Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Mamlaka husika.

Maombi yaliyowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili hayatafikiriwa.

Maombi yote yatumwe kwenye Anuani ifuatayo ;

MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.L.P 27,
SINGIDA.

N.B: Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10/03/2025.

DOWNLOAD PDF HAPA

Leave a Comment