TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI NA MSINGI KWA MWAKA WA MASOMО 2025/2026
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) anatangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi. Mafunzo yatakayotolewa ni Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (Miaka 02) pamoja na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi na Hisabati. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali Msingi na Elimu Maalumu (miaka 02) ni wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III).
Waombaji wa nafasi za mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi na Hisabati ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Mafunzo haya yatatolewa katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali. Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
a) Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) ni: b) (i) Wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02). Aidha, kwa waombaji waliosomea masomo ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali.
(ii) Walimu waliohitimu Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Awali au Msingi. Aidha waombaji wa mafunzo watakaochaguliwa, watapangwa kwenye mikondo kulingana na ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada ya Elimu ya Ualimu.
Sifa za kujiunga na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, mawili kati yake yakiwa ni: Basic Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer Studies au Computer Science.
DOWNLOAD PDF HAPA CHINI
Leave a Comment