Chuo cha JKT kimewakaribisha vijana waliohitimu darasa la saba kujiunga na mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku.
Wito huo umetolewa leo Jumamosi Julai 5, 2025 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT), Kanali Shija Lupi, alipokuwa akizungumza katika maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DiTF), maarufu Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kanali Lupi amesema kuwa JKT kupitia chuo chake cha mafunzo kilichopo Mgulani, kinapokea vijana kuanzia waliohitimu darasa la saba na kuendelea, kwa lengo la kuwapatia stadi za ufundi zitakazowasaidia katika maisha yao ya kila siku.
Katika hatua nyingine, wananchi wamevutiwa na teknolojia ya ufugaji wa samaki kwa kutumia matenki.
Kanali Lupi amesema teknolojia hiyo imeanzishwa na Suma JKT na wananchi watakaotembelea banda lao watapata fursa ya kujionea kwa karibu ufugaji huo, pamoja na kufundishwa na wataalamu waliobobea katika sekta hiyo.
Leave a Comment