NECTA: Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 (Form Four Results). Baraza la Mitihani Tanzania linatarajiakutangaza matokeo ya Mtihani wa kidato cha Nne 2022, uliofanyika mwezi novemba 2024. Matokeo haya huwapa wanafunzi, wazazi, na jamii kwa ujumla picha kamili ya uwezo wa mwanafunzi na mafanikio yake kitaaluma. Makala haya yanalenga kutoa taarifa muhimu na za kina kuhusu mtihani wa kidato cha nne, malengo yake, sifa za kujiunga, masomo yanayofanyiwa mtihani, na muhimu zaidi, jinsi ya kuangalia matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2024.
Lini Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 Yanatarajiwa Kutangazwa?
Ni vigumu kuwa na taarifa rasmi za Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kuhusu tarehe ya kutangazwa kwa matokeo ya Kidato cha Nne 2024. Wanafunzi na wazazi wanashauriwa kufuatilia tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz) kwa taarifa za uhakika
Hata hivyo, kutokana na desturi za mwaka jana na miaka mingine iliyopita, ni wazi kwamba matokeo haya yanatarajiwa kutangazwa mwezi Januari 2024. Kwa mfano:
2023: Matokeo ya Kidato cha Nne yalitangazwa Januari 25.
2022: Matokeo yalitangazwa Januari 29.
2021: Matokeo yalitangazwa Januari 15.
2020: Matokeo yalitangazwa Januari 15.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Nne 2024
1. Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA anwani: www.necta.go.tz.
2. Chagua Sehemu ya “Results” (Matokeo ya Mitihani)
Baada ya kufungua tovuti, bofya kitufe cha Results kinachoonekana kwenye menyu kuu. Hii itakufikisha kwenye orodha ya mitihani yote inayosimamiwa na NECTA.
3. Chagua “CSEE” (Certificate of Secondary Education Examination)
4. Chagua Mwaka wa Mtihani
Baada ya kufungua ukurasa wa CSEE, utaona miaka ya matokeo iliyoorodheshwa. Tafuta na chagua mwaka husika, yaani, 2024.
5. Tafuta Jina la Shule
Mara baada ya kuchagua mwaka, utaelekezwa kwenye orodha ya shule zote zilizoshiriki mtihani huo. Tumia kipengele cha utafutaji kutafuta jina la shule yako ili kuonyesha matokeo ya wanafunzi wote wa shule hiyo.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 Kupitia Mfumo wa SMS
1. Fungua sehemu ya kuandika ujumbe kwenye simu yako.
2. Andika ujumbe huu: CSEE ikifuatiwa na namba ya mtihani wa mwanafunzi (mfano: CSEE 12345678910).
3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15300.
4. Utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo ya mwanafunzi mara tu ujumbe wako utakaposambazwa na kupokelewa.
Leave a Comment