Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, NIDA inatarajia kusitisha matumizi ya namba za vitambulisho vya NIDA kunanzia Mei 1, mwaka huu, kwa wananchi wote waliotumiwa ujumbe mfupi (SMS), kwenda kuchukua vitambulisho vyao na hawajafanya hivyo.
Akizungumza mapema leo ofisini kwake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji amesema NIDA imesikitishwa na idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza kuchukua vitambulisho vyao.
“Inasikitisha sana, tumekuwa tukituma ujumbe mfupi kwa wananchi kuwaelekeza ni mahali gani waende kuchukua vitambulisho vyao lakini idadi ni ndogo sana.
“NIDA tumeamua kuwa tutasitisha matumizi ya namba za vitambulisho, kwa wale wote ambao wameshatukiwa vitambulisho lakini hawajachukua,” amesema Kaji.
Katika hatua nyingine, Kaji amesema NIDA ipo katika hatua za mwisho katika kuja na mfumo mpya wa kusajili kuanzia watoto wadogo.
Leave a Comment