NYARAKA AMBAZO MWANAFUNZI ANATAKIWA KWENDA NAZO CHUONI;
1. Mwanafunzi anatakiwa kuripoti akiwa na vyeti halisi vya elimu na fani mbalimbali. Mwanafunzi ambaye hatokuwa na nayaraka halisi hatapokelewa chuoni. Vyeti na Nyaraka zinazotakiwa ni kama ifuatavyo:-
2. Cheti cha kuzaliwa,
3. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba,
4. Vyeti halisi (Original) vya Elimu ya Kidato cha Nne, cha Sita na Shahada,
5. Vyeti vya Ujuzi wa aina mbalimbali (Kwa wale wenye ujuzi).
VIFAA NA MAHITAJI AMBAYO MWANAFUNZI ANATAKIWA KWENDA NAYO CHUONI
Fedha kiasi cha Tshs. 50,400/= kwa ajili ya Bima ya Afya kwa asiyekuwa na Kadi ya Bima ya Afya au mwenye Kadi ya Bima ya Afya ambayo inaisha uhai wake kabla ya tarehe 31/12/2025, Fedha kiasi cha Tshs. 25,000/= kwa ajili ya vipimo vya afya, Fedha za kujikimu kwa ajili ya matumizi binafsi, Truck suit (02) rangi nyeusi na dark blue, Raba za michezo jozi (02) rangi yoyote, Nguo nadhifu za kiraia jozi (03), Mashuka (04) rangi ya bluu, Mto wa kulalia (01), Foronya (02) rangi ya bluu,
Chandarua (01) rangi ya bluu, Madaftari makubwa (04) 4QRs, Sanduku la chuma (Trunker), Ndoo (02) za plastiki (moja ya lita 10 na moja ya lita 20), Fulana (02) rangi ya dark blue zenye shingo ya duara, Viatu vya mvua (rainboot,) jozi (01), Taulo (01), Kandambili jozi (01) pamoja na Vifaa vya Usafi ikiwemo Jembe (01) na mpini wake, Fyekeo (01), Panga (01) na Rake (01).
Leave a Comment