TAARIFA KWA UMMA
KUITWA KUANZA MAFUNZO YA UFUNDI NA STADI ZA KAZI KATIKA FANI MBALIMBALI KWA NJIA YA UANAGENZI
Itakumbukwa kuwa tarehe 31 Januari, 2025 Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) ilitangaza fursa za mafunzo ambayo yatatolewa katika Taasisi za mafunzo zilizotangazwa. Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inapenda kuutaarifu umma kuwa jumla ya vijana 8,000 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo katika vyuo 52 nchini. Majina ya vijana waliochaguliwa yamebandikwa kwenye mbao za matangazo za vyuo husika na katika tovuti ya www.kazi.go.tz. Vijana waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo hivyo kwa ajili ya kujisajili kuanza mafunzo kuanzia tarehe 3 Machi, 2025.
Leave a Comment