Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Orodha ya Vyuo Vilivyoruhusiwa Kufanya Udahili Machi Intake 2025

Orodha ya Vyuo Vilivyoruhusiwa Kufanya Udahili Machi Intake 2025

Baraza linapenda kuufahamisha umma kuwa udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi zote utaanza tarehe 10 hadi 28 Februari, 2025. Udahili katika muhula huu wa Machi, 2025 utahusisha vyuo vilivyo na nafasi na uwezo wa kupokea wanafunzi wapya isipokuwa vya afya kwa Tanzania Bara.

Aidha, wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada wanashauriwa kutuma maombi yao ya kudahiliwa moja kwa moja vyuoni. Waombaji watakaochaguliwa na vyuo watakavyoomba watawasilishwa NACTVET kwa ajili ya uhakiki kabla ya kufahamishwa kujiunga na mafunzo.

Masomo kwa watakaochaguliwa na kuhakikiwa yataanza tarehe 07 Aprili, 2025.

Baraza linavishauri vyuo na taasisi zote zitakazodahili wanafunzi kwa Muhula wa Machi, 2025 kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu za matukio ya udahili kama zilivyo kwenye Kalenda ya Udahili (Admission Calendar) inayopatikana kwenye tovuti ya Baraza.

Pia Baraza linawashauri waombaji na wazazi kuhakikisha kuwa wanafanya maombi kwenye vyuo
vilivyokidhi vigezo na kuruhusiwa kudahili katika muhula wa Machi, 2025 na vimeorodheshwa kwenye
tangazo hili.

Download orodha ya vyuo vilivyoruhusiwa kufanya udahili wa Machi 2025 hapa chini

UDAHILI WA WANAFUNZI KATIKA MKUPUO WA MACHI 2025/2026

Leave a Comment