The application window for 2025/2026 Samia Scholarship opens once form six results for 2025 examinations are out and names of successful candidates are submitted to HESLB for further steps.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza programu ya Ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2025 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN).
SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja (100%) masomo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.
SIFA ZA KUPATA UFADHILI
Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye sifa zifuatazo:
1. Awe Mtanzania;
2. Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2023 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi;
3. Awe amepata udahili katika Chuo cha Elimu ya Juu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali katika programu za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati au Tiba ambazo zimetajwa katika kundi la kwanza (Cluster 1) katika Mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2023/2024 unaopatikana kupitia www.heslb.go.tz
4. Awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa.
MAENEO YA UFADHILI
Ufadhili utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya kugharamia maeneo yafuatayo:
a. Ada ya Mafunzo
b. Posho ya chakula na malazi
c. Posho ya Vitabu na Viandikwa
d. Mahitaji Maalum ya Vitivo
e. Mafunzo kwa Vitendo
f. Utafiti
g. Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu
h. Bima ya Afya
MUDA WA UFADHILI
Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharimiwa kati ya miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.
5.0 UTARATIBU WA KUOMBA UFADHILI
Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz.
DOWNLOAD PDF WANAFUNZI 100 WA KIDATO CHA SITA 2025 WENYE SIFA YA KUOMBA SAMIA SCHOLARSHIP
Leave a Comment