Sifa za Jumla Kwa Wanafunzi wanaojiunga na Vyuo
Uraia: Mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania.
Umri: Mwombaji ashindwe miaka 35 wakati wa kuomba mkopo.
Udahili: Ni sharti mwombaji awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu ya juu nchini Tanzania inayotambuliwa.
Maombi kupitia OLAMS: Maombi yote ya mkopo yanafanywa kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS).
Ukosefu wa kipato: Mwombaji hapaswi kuwa na chanzo kingine cha mapato, kama vile ajira au mkataba serikalini au sekta binafsi.
Kurejesha mkopo uliopita: Kwa wale ambao wameshawahi kupokea mkopo wa HESLB, ni lazima wawe wamerejesha angalau asilimia 25 ya mkopo huo kabla ya kuomba tena.
Ufaulu wa masomo: Waombaji wanatakiwa wawe wamehitimu elimu ya kidato cha sita au stashahada ndani ya miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi 2024.
Sifa za Msingi kwa Wanafunzi Wanaondelea na Masomo
Kwa wanafunzi ambao tayari wako vyuoni na wanataka kuendelea kupata mkopo, au wale wanaotaka kuomba mkopo kwa mara ya kwanza wakiwa wanaendelea na masomo, wanatakiwa kutimiza yafuatayo:
Ufaulu: Ni lazima wawe wamefaulu mitihani yao ili waweze kuendelea na mwaka unaofuata wa masomo.
Barua ya kurejea (kama inafaa): Kwa wale waliowahi kuahirisha masomo, wanapaswa kuwa na barua ya kurejea masomoni kutoka chuo husika.
Kurudia mwaka: Wanafunzi hawaruhusiwi kurudia mwaka wa masomo zaidi ya mara moja katika kipindi chote cha masomo yao.
Kuahirisha masomo: Hairuhusiwi kuahirisha masomo kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo.
Namba ya Utambulisho ya Taifa (NIN) na namba ya usajili: Lazima wawasilishe namba hizi kabla ya kupokea fedha za mkopo katika mwaka wao wa tatu wa masomo.
Leave a Comment