Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Sifa za Kujiunga JKT - Jeshi la Kujenga Taifa

Sifa za Kujiunga JKT – Jeshi la Kujenga Taifa

Fahamu Sifa za Kujiunga JKT Tanzania: Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo:

Awe raia wa Tanzania

Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..

Awe hajaoa/hajaolewa

Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25

Awe na tabia na mwenendo mzuri

Awe na akili timamu na afya nzuri

Masharti ya Utumishi

Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.

Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.

Maafisa

Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili Askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za Askari wapya (Recruitment Schools).

Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya Uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.

Dhima ya JWTZ

Kulinda nchi na kutetea maslahi ya Taifa la Tanzania, kutoa msaada kwa Mamlaka za kiraia na kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya Kitaifa na Kimataifa.

Majukumu ya Msingi ya JWTZ

• Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

• Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

• Kufanya Mafunzo na Mazoezi ili kujiweka tayari Kivita wakati wote.

• Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.

• Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa.

• Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

• Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.

Leave a Comment