Kozi ya Uhandisi wa vifaatiba (Biomedical engineering)
Biomedical engineering ni kozi itakayokuwezesha kutengeneza, kudizaini na kufanyia marekebisho vifaatiba vinavyotumika katika vituo vya afya.
Wahitimu wa kozi hii wanaweza kufuata njia tofauti za kazi katika sekta ya afya. Wana uwezo wa kufanya kazi kama wataalamu wa matengenezo na upimaji wa vifaa tiba katika hospitali na kliniki, au kama washauri wa usimamizi wa vituo vya afya. Zaidi ya hayo, wanaweza kuajiriwa na makampuni yanayosambaza vifaa tiba, au kuendeleza taaluma zao zaidi kwa kujiunga na taasisi za elimu ya juu kwa shahada.
Baadhi y vyuo vinavyotoa kozi ya Uhandisi wa vifaatiba (Biomedical engineering)
Mvumi Institute of Health Sciences
Dar es Salaam Institute of Technology
Arusha Technical College – Arusha
Sifa za Kujiunga na kozi ya Uhandisi wa vifaatiba (Biomedical engineering)
Mwanafunzi anatakiwa awe na Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) na angalau alama nne (4) za kupita katika masomo yasiyo ya kidini ikiwa ni pamoja na Kemia, Baiolojia, na Fizikia/ Sayansi za Uhandisi.
Biology D
Chemistry D
Physics D
English D
Na ufaulu zadi ya huo Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
Leave a Comment