Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Taarifa Mpya Kuhusu Ajira za Jeshi la Uhamiaji 2025

Taarifa Mpya Kuhusu Ajira za Jeshi la Uhamiaji 2025

TAARIFA KWA UMMA

Hivi karibuni Idara ya Uhamiaji ilitoa tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya Uhamiaji vijana wa Kitanzania kupitia tovuti na mitandao yake ya kijamii (Instagram, Twitter, Facebook).

Kufuatia tangazo hilo, kumekuwepo na Matapeli wanao walaghai Wananchi kupitia mitandao ya kijamii na baadhi yao kuwapigia simu au kuwatumia ujumbe kwa njia ya sms kwamba kuna nafasi za ajira na kuwataka kutuma fedha ili wawasaidie kupata nafasi hizo za ajira.

Idara inapenda kuufahamisha Umma kuwa mchakato huo wa ajira ulishakamilika na uliendeshwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za ajira kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la ajira. Hivyo, Wananchi wanaombwa kupuuza na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe huo.

Taarifa rasmi za Idara kuhusu ajira na nyinginezo, hutolewa kupitia mifumo rasmi ya mawasiliano ikiwemo Vyombo vya Habari, tovuti ya Idara ambayo ni www.immigration.go.tz na mitandao yake ya kijamii (@UhamiajiTz).

Aidha, Idara ya Uhamiaji inaendelea na uchunguzi kwa lengo la kuwabaini wanaohusika na uhalifu huo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Imetolewa na;

SSI. Paul J. Mselle
MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI

Leave a Comment