TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA AJIRA ZA UALIMU KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kutokana na upotoshaji unaoendelea kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamiikuhusu mchakato wa ajira za walimu unaoendelea katika Mikoa yote nchini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeona upo umuhimu wa kutoa ufafanuzijuu ya suala hili.
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kama sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma, kifungu cha(4.2)(ii)(iii) inayoelekeza kuwa: Ajira za ushindani zifanyike katika madaraja ya kuingilia kwenye miundo ya utumishi; na Kiundwe chombo cha ajira katika Utumishi wa Umma kitakachokuwa kinashughulikia na kusimamia upatikanaji wa wataalamu
mbalimbali. Katika kuwezesha utekelezaji wa Sera hii, Kifungu cha 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298, kinaelekeza kuwepo kwa chombo maalumu cha kushughulikia mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma. Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma za Mwaka 2021 zilizotolewa
kupitia Tangazo la Serikali Na.580 la Mwaka 2022 ndizo zinazozingatiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la Mwaka 2023, kifungu cha (3.12.1.5) inaelekeza kuwa: Serikali itaimarisha mfumo wa ajira ya walimu, wakufunzi, na wahadhiri kwa kuhakikisha kuwa wenye sifa na viwango stahiki wanaajinwa baada ya kufanya mitihani na kufaulu kama sehemu ya usaili.





Leave a Comment