Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
TAMISEMI Form Five Selection Katavi 2025/2026

TAMISEMI Form Five Selection Katavi 2025/2026

Majina Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2025 na Vyuo vya Kati Mkoa wa Katavi  . Selection Form Five au form five slection ni utaratibu uliowekwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET).

Mchakato huu unahusisha uchaguzi wa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano na vyuo vya kati na vya ufundi kwa mwaka husika.

Kabla ya matokeo ya Form Five Selection, TAMISEMI hutoa nafasi ys wanafunzi kubadi au kuongeza machaguo ya shule, tahasusi na vyuo kulingana na ufaulu waliopata katika matokeo ya kidato cha nne kupitia mfumo wa Selform TAMISEMI.

Jinsi ya Kutumia Mfumo wa TAMISEMI SELFORM

Ukiwa kwenye internet, fungua kivinjari chako (browser mfano, chrome), andika anuani ifuatayo selform.tamisemi.go.tz kupata dirisha la kujaza taarifa zako za kujisajili kama inavyoonekana hapo chini. Bofya Menu ya chini kabisa iliyoandikwa For Candidates, Click here to Register kama mtumiaji ni mara yake ya kwanza.

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

Kisha, ujaze taarifa zinazohusika za Index Number kwa format ya Mfano S0101.0020.2018, Jibu swali utakaloulizwa, Jina la Ukoo na Mwaka wa kuzaliwa kama inavyoonekana hapo chini.

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

Kisha dirisha litafunguka na kutaka ujaze Password utakayoitumia siku zote. Dirisha lifuatalo litafunguka;

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

Ukishaandika Password, mfumo utaonekana katika sura hii kuonesha umefanikiwa kubadili Password;

Ukishabadili Password, utaitumia kuingia kwa mara nyingine kwa kuandika username

mfano S0101.0002.2018 na Password uliyoibadili.

Jinsi ya Kubadili Combinations 2025/2026 - Selform Tamisemi

PART A: TAARIFA BINAFSI ZA MWANAFUNZI

Ukishaingia kwenye mfumo, dirisha lifuatalo litafunguka na sehemu zilizozungushiwa tu ndio utaweza kubadili taarifa binafsi. Ukimaliza kujaza bofya Save and Next hapo chini ili kuendelea mbele.

C:\Users\mtatifikoloj\Downloads\Capture 2019-03-27 at 19.10.04.png

PART B1: STUDENT GENERAL CHOICES

Bofya katika sehemu hii ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo.

PART B2: ALTERNATIVE OPTIONS

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya vyuo vya Kisekta. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT.

PART C1: FORM V STUDENT DETAILED CHOICES

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya shule za form V na tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi ataona Possible combinations tu na shule kutokana na ufaulu wa matokeo yake kwa lengo la kubadilisha. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C2: TECHNICAL EDUCATION

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Technical na Tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi lazima awe na ufaulu wa Tahsusi ya PCM katika matokeo yake kwa ajili ya kubadilisha eneo hili. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C3: HEALTH EDUCATION

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Afya na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C4: DIPLOMA EDUCATION

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Elimu na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

PART C5: OTHER COLLEGES

Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo Vinginevyo na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.

Jinsi ya Kuangalia Uchaguzi wa Wanafunzi Kidato cha Tano 2025/2026

1. Nenda moja kwa moja kwenye tovuti ya TAMISEMI: http://tamisemi.go.tz./ au https://selection.tamisemi.go.tz/

2. Bofya kiungo rasmi cha Matokeo. (https://selform.tamisemi.go.tz/)

3. Chagua mkoa, kisha wilaya

4. Angalia jina la shule yako kutoka kwenye orodha ambayo itawasilishwa.

5. Tembeza chini ili kuangalia “majina ya selection kidato cha tano 2025/2026”.

Unaweza Kutumia hii link Kupata Mateo ya Uchaguzi (Form Five & Vyuo)

Leave a Comment