Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Tangazo la Kuitwa Kazini Wizara ya Afya 2025

Tangazo la Kuitwa Kazini Wizara ya Afya 2025

TANGAZO LA KUITWA KAZINI WIZARA YA AFYA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya anapenda kuwataarifu waombaji wote waliofaulu usaili wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na kupangiwa kuripoti Wizara ya Afya kwamba, waripoti katika Ukumbi wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi, Mirembe DODOMA ( DIHAS) ili kukamilisha taratibu za ajira kama tarehe zinavyoonesha kwenye tangazo. Waajiriwa wote wanatakiwa kufika na vyeti halisi (Original) nakala 2 kwa kila cheti ambacho kilitumika wakati wa kuomba ajira ikiwa ni pamoja na:

Nakala ya cheti cha kuzaliwa.

Wasifu binafsi (CV).

Picha mbili (2) Passport size.

Nakala ya Kitambulisho/namba ya uraia (NIDA).

Nakala ya vyeti vya elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne na Sita).

Nakala ya vyeti vya taaluma pamoja na Transcript.

Nakala ya Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo. (Internship).

Nakala ya cheti cha usajili kutoka Baraza na Bodi husika (Valid Licence).

Nakala ya Ithibati ya vyeti vya elimu na taaluma (Accreditation and Equivalence) kutoka TCU na NECTA kwa waliosoma vyuo vya nje ya nchi pamoja na wale waliosoma Sekondari nje ya nchi/Mitaala ya nje.

Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa hakikisha unawasilisha Kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa
Msajili wa Viapo na kusajiliwa na Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Kuripoti vituo vya kazi watakavyopangiwa katika muda wa siku 14 baada ya kupokea barua ya ajira. Waajiriwa watakaoshindwa kuripotikatika vituo
walivyopangiwa kwa muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika.

Aidha, yeyote atakayeripoti na Transcript tu au kuwa na nakala pungufu za vielelezo tajwa hapo juu hatapokelewa.

Download PDF Orodha ya majina ya Walioitwa Kazini.

Leave a Comment