Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Tangazo la Nafasi 8,000 za Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Fani Mbalimbali

Tangazo la Nafasi 8,000 za Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Fani Mbalimbali

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 52 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi ambavyo vimesajiliwa na Mamlaka husika kutoa mafunzo katika fani mbalimbali zikijumuisha ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashi, Useremala, Uchomeleaji na uungaji vyuma, Upakaji rangi
na maandishi ya alama, Upishi, Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi Magari na Mitambo, umeme wa majumbani na viwandani, Umeme wa Magari, Huduma za Hoteli na Utalii, Ukataji Madini na Ufundi vyuma.

Ofisi inapenda kuwatangazia vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani zilizoorodheshwa hapo chini wafike katika vyuo vya VETA vya Mikoa na Wilaya pamoja na vyuo vilivyoainishwa hapa chini ili kuchukua fomu ya kuomba kujiunga na mafunzo. Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi / mzazi / mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani. Mafunzo yataanza tarehe 03 Machi, 2025 na yatakua ya kutwa. Mwombaji anashauriwa kuomba mafunzo haya katika chuo kilicho katika Mkoa anaoishi.

Leave a Comment