Tetesi za usajili Ligi Kuu kuelekea msimu mpya NBC Premier League Tanzania 2025/2026: Dirisha la usajili bado lipo wazi mpaka tarehe 15/8/2024, Timu mbalimbali bado zinafanya jitihada za kuimarisha vikosi vyao maeneo mbalimbali.
Simba ndio timu ambayo imeongoza kwa kusajili idadi kubwa ya wachezaji, zaidi ya wachezaji kumi huku bado ikiwa inahusishwa katika tetesi mbalimbali kuelekea mwishoni mwa dirisha la hili la usajili.
Moussa Pinpin Camara
Ayoub Lakred golikipa namba moja wa Simba SC amepata majeruhi, anatajwa kukaa njee kwa muda mrefu. Simba imeona ni busara kutafuta mbadala wa nafasi hiyo Moussa Pinpin (Guinea) kutoka Klabu ya Horoya AC.
Kibu Denis
Klabu ya Kristiansund BK imeandika barua rasmi kwenda Simba SC ili kumnunua mchezaji huyo kwa kuzingatia kipengele hicho kilichopo kwenye mkataba wa mchezaji huyo. Somba inahaha kutafuta mbadala wa Kibu katika kikosi. Simba ipo mbioni kunasa saini ya Elie Mpanzu wa AS Vita, kama mbadala wa Kibu.
Elie Mpanzu
Elie Mpanzu Kibisawala ni raia wa Congo DR anayeitumikia klabu ya AS Vita Club. Simba imehusishwa na Mpanzu kwa ukubwa zaidi baada ya Kibu Denis kuonyesha dalili za kutokuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao.
Leave a Comment