TOTO AFYA ni kifurushi cha bima ya afya ni kwa ajili ya watoto walio chini ya miaka 18 ambao watachangia na kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima katika vituo vilivyosajiliwa na Mfuko kuhudumia wanachama wake. TOTO AFYA iko kwa namna mbili za usajili ambazo ni :-
(i) Kujiunga kwa makundi kupitia Shule za Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Kati na Vikuu
(ii) Kujiunga mtoto mmoja mmoja.
Faida za kujiunga na Toto Afya
· Wigo mpana wa huduma za msingi, kibingwa na kibingwa bobezi.
· Matibabu nchi nzima katika vituo vya matibabu zaidi ya 10,000 kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitalii ya Taifa. Aidha utaratibu wa rufaa utatumika katika Hospitiali za Kanda na Taifa.


Viwango vya uchangiaji
Mchango wa Toto Afya kwa watoto watakaojiunga kwa makundi ya Shule au Vyuo ni TZS 50,400/- kwa mnufaika kwa mwaka. Mchango wa Toto Afya kwa watoto watakaojiunga mmoja mmoja ni TZS 150,000/- kwa mnufaika kwa mwaka.
Mambo muhimu ya kuzingatiwa kabla ya kujiunga na Toto Afya: –
Mahitaji ya watoto wanaojiunga kwa makundi kupitia Shule za Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu :-
a) Picha moja ya rangi.
b) Namba ya usajili shuleni (PREM Number) kwa wanafunzi wa Shule za Awali, Msingi na Sekondari na (Registration Number) kwa wanafunzi Vyuo vya Kati na Vikuu.
c) Namba ya simu ya mzazi au mlezi kwa wanafunzi wenye umri chini ya miaka 18.
Namba ya simu ya mkononi kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 18 au zaidi walio na d)
e) Namba ya Kitambulisho cha Uraia (NIN) kwa wanafunzi waliopatiwa namba hizo.
f) Watoto watakaosajiliwa kupitia shule au vyuo au vituo vya kulelea watoto watakuwa na tarehe moja ya kuanza na kuisha kwa muda wa matumizi.
Mahitaji kwa watoto watakaojiunga mmoja mmoja: –
a) Picha moja ya rangi.
b) Nakala ya cheti cha kuzaliwa kilichohakikiwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).
Namba ya simu ya Mzazi/Mlezi/Mdhamini.
d) Wanachama wanaosajiliwa mmoja mmoja watakuwa na muda wa kusubiri wa siku 90 kabla ya kuanza kupata huduma.
Mdhamini atajaza fomu ya taarifa za afya ya mtoto kwa watoto walioandikishwa mmoja mmoja (Health Assessment Form).
Kila mwanachama atakuwa na ukomo wa gharama za huduma kwa mwaka hivyo wanachama wanashauriwa kufuatilia matumizi yao kwa ukaribu na kuepuka matumizi holela.
Namna ya Kujisajili
Watoto wanaojiunga kwa makundi kupitia Shule za Awali, Msingi na Sekondari Shule itasajiliwa na Mfuko katika mfumo wa wanachama ili iweze kuandikisha wanafunzi katika bima ya afya.
Baada ya kujaza taarifa muhimu, shule au mzazi au mlezi atapokea namba ya malipo (control number) ambayo ataitumia kufanya malipo kupitia benki au mitandao ya simu.
Mzazi au shule itafanya malipo kwa mkupuo (Full Payment).
Mwanachama atapatiwa namba ya kitambulisho au nakala ya kitambulisho cha matibabu cha kielekroniki (e-Card) na kwa wale wenye namba za kitambulisho cha Taifa wanaweza kupata huduma kupitia kitambulisho hicho.
Namna ya Kujisajili
Watoto wanaojiunga kwa makundi kupitia Shule za Awali, Msingi na Sekondari Shule itasajiliwa na Mfuko katika mfumo wa wanachama ili iweze kuandikisha wanafunzi katika bima ya afya.
Baada ya kujaza taarifa muhimu, shule au mzazi au mlezi atapokea namba ya malipo (control number) ambayo ataitumia kufanya malipo kupitia benki au mitandao ya simu.
Mzazi au shule itafanya malipo kwa mkupuo (Full Payment). Mwanachama atapatiwa namba ya kitambulisho au nakala ya kitambulisho cha matibabu cha kielekroniki (e-Card) na kwa wale wenye namba za kitambulisho cha Taifa wanaweza kupata huduma kupitia kitambulisho hicho.
Watoto wanaojiunga kwa makundi kupitia Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu Vyuo vinasajiliwa katika mfumo wa NHIF ili kuandikisha wanafunzi kwa bima ya afya.
Baada ya chuo kusajiliwa, mwanafunzi au chuo kitapokea namba ya malipo (control number) itakayotumika kufanya malipo kupitia benki au mitandao ya simu.
Mwanafunzi au chuo atafanya malipo kwa mkupuo (Full Payment). Mwanachama atapatiwa namba ya kitambulisho au nakala ya kitambulisho cha matibabu cha kielekroniki (e-Card) na kwa wale wenye namba za kitambulisho cha Taifa wanaweza kupata huduma kupitia kitambulisho hicho.
Kwa maelezo zaidi, tembelea Ofisi ya NHIF iliyo karibu nawe au piga simu bila malipo namba 199.
Leave a Comment