Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
UMEMALIZA KIDATO CHA NNE? SOMA HII

UMEMALIZA KIDATO CHA NNE? SOMA HII

UMEMALIZA KIDATO CHA NNE NA UNANDOTO ZA KUSOMA KOZI ZA AFYA? SOMA HII.

NI UKWELI USIOFICHIKA ufaulu unaongezeka, ushindani umeongezeka kuanzia kwenye kupata chuo/shule ya kusoma hadi kwenye kutafuta ajira!.

Wahitimu wengi wa kidato cha nne wenye ndoto za kusoma kozi za AFYA mfano MD na Pharmacy, njia rahisi ilikuwa ni kusoma advance na kujiunga na chuo (Degree).

Ilikuwa rahisi, ila kwa sasa ushindani umeongezeka, TCU wamebana kuanzia kwenye entry qualifications, CBG sio tahasusi inayokuwezesha kusoma kozi za AFYA! kwasasa.

Bado licha kusoma combination husika kama PCB, imekuwa ni ngumu kupata nafasi kujiunga na kozi za Afya kama MD na Pharmacy. Mwanafunzi anakuwa na Division 1 ya point 8 form six lakini anaomba kozi za afya (degree) anatemwa kutokana na ushindani.

Wengine wanatamani hata kurudi tu wasome diploma licha ya kumaliza form six, maana wanakosa nafasi za kusoma kozi za afya, kama sehemu ya ndoto zao!.

TUPITIE WAPI SASA?

Well, njia ni rahisi ila inagharama, kama familia yako inaweza kukusomesha, usiende form 5 & 6 nenda kasome diploma kozi ya ndoto yako, naamini hutajutia.

Faida

Ukisoma Diploma unauwezo wa kuendelea na degree, lakini muda huo ukiendelea kuomba kazi kwa cheti cha diploma.

Faida ya pili, risk ni ndogo ya kufeli diploma na utasomea professional.

Tatu, diploma unanafasi ya kujifunza vingi na kubobea. Waajiri wengi wanapenda watu waliopita diploma.

By Waza Elimu

Leave a Comment