Majina ya Miundo na Ngazi ya Mishahara ya kwa Watumishi Serikali 2025/2026. Serikali inaendelea kutekeleza Sera ya malipo ya Mshahara na Motisha katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2010. Katika hatua za kutimiza malengo ya Sera hii, Serikali imefanya marekebisho ya mishahara ya watumishi wake kuanzia tarehe 1 Julai, 2022. Kufuatia marekebisho hayo, kima cha chini cha mshahara kimeongezwa kwa asilimia 23.3 kutoka shlingi 300,000 kwa mwezi hadi shilingi 370,000 kwa mwezi. Ngazi nyingine za mshahara zimeongezwa kwa asilimia tofauti.
Kutokana na mabadiliko haya, upeo wa ngazi za mishahara iliyotolewa kwa Waraka wa Watumishi wa Serikali Na. 1 wa mwaka 2015, sasa utakuwa kama ilivyooneshwa katika Viambatanisho Na. 1 – 11 vya Waraka huu. Aidha, vianzia mshahara kwa msingi wa Elimu, Muda wa Mafunzo, aina ya kazi na ujuzi vitakuwa kama vilivyoainishwa katika Miundo ya Maendeleo ya Utumishi ya kada husika pamoja na miongozo mbalimbali iliyotolewa na Ofisi hii.
Wanaohusika na Marekebisho haya ya mshahara
Serikali za Mitaa, watumishi walioshikizwa kwenye Taasisi za Umma pamoja na watumishi ambao watakuwa kwenye likizo inayoambatanana na kuacha kazi au kustaafu kazi baada ya tarehe 1 Julai, 2022.
Watumishi Wanaopata Mishahara Binafsi
Watumishi ambao wanapata mishahara binafsi (Personal Salaries) iliyo ndani ya viwango vya mishahara ya Serikali na ambayo ni mikubwa kuliko ile ya vyeo vyao halisi (Substantive Post) Serikalini, watahusika na marekebisho haya iwapo vyeo na
Marekebisho haya yanawahusu watumishi wa Serikali Kuu, watumishi wa mishahara yao itaangukia katika vyeo na ngazi mpya za mishahara. Aidha, watumishi wanaopata mishahara binafsi isiyo ndani ya viwango vya mishahara ya Serikali hawatahusika na marekebisho haya.
Tarehe ya Mabadiliko
Watumishi wa Serikali Na. 1 wa Mwaka 2015. Waajiri wote wanaohusika na Waraka huu wanatakiwa kurekebisha mishahara ya watumishi wao kulingana na viwango vilivyotolewa katika Waraka huu.
Waraka huu ni kumbukumbu na taarifa ya Serikali na hairuhusiwi kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
PAKUA PDF HAPA CHINI
Leave a Comment