Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa Tuzo kwa washindi msimu uliopita 2023/2024.
Mfungaji Bora wa Ligi
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki ametangazwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.
Golikipa Bora, Kombe la Shirikisho (CRDB)
Mlinda mlango wa klabu ya Yanga Sc, Djigui Diarra ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Michuano ya FA (CRDB FEDERATION CUP).
Golikipa Bora, Ligi Kuu Bara
Mlinda mlango wa Coastal Union, Ley Matampi ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara Msimu wa 2023/2024 akiwashinda Djigui Diarra wa Yanga na Ayoub Lakred wa Simba SC.
Beki Bora Ligi Kuu Bara
Beki wa Yanga Sc na Timu ya taifa ya Tanzania, Ibrahim Bacca ameshinda tuzo ya beki Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.
Kiungo Bora
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki.
Mchezaji Bora wa Tanzania, Anayecheza Nje
Mbwana Samatta.
Mfungaji Bora (MVP) kombe la Shirikisho
Kiungo wa Azam Fc, Faisal Salum ‘Feitoto’ ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa kombe la Shirikisho la CRDB (CRDB Federation Cup 2023/24)
- Mchezaji Bora Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) – Aisha Mnunka
- Mfungaji Bora Ligi ya Wanawake – Aisha Mnunka
- Kipa Bora Ligi ya Wanawake – Caroline Rufo
Leave a Comment