1. Atakuwa Mwalimu Mkuu Msaidizi
2. Atamwakilisha Mwalimu Mkuu katika shughuli mbalimbali kila inapolazimu pamoja na kushughulikia kazi mbalimbali za Mwalimu Mkuu wakati akiwa hayupo kituoni pake.
3. Atakuwa kiungo kati ya Mwalimu Mkuu na walimu. Atatakiwa kumpa Mwalimu Mkuu taarifa mbalimbali zinazohusu maoni na matatizo ya walimu hasa kuhusu uendeshaji wa shule kwa ujumla.
4. Atashughulikia masuala yote yanayohusu nidhamu shuleni na kuweka kumbukumbu za adhabu na maonyo yote yatolewayo katika kitabu maalum. Katika kutekeleza wajibu huu atashauriana na Mwalimu Mwandamizi anayeshughulikia malezi ya wanafunzi shuleni, kamati ya nidhamu na walimu wote kwa ujumla.
5. Atasimamia na kuongoza kazi zote za Halmashauri ya Shule kwa kushirikiana na Mwalimu Mkuu.
6. Atashughulikia mipango ya uingizaji wa wanafunzi shuleni, pia mahudhurio yao.
7. Atahakikisha kuwa shule ina utaratibu wa utekelezaji wa shughuli zote.
8. Atasimamia utendaji kazi wa wafanyakazi wote wasio walimu.
9. Atapokea wageni mbalimbali wanaowahusu wanafunzi.
10. Atashughulikia mipango ya matumizi ya gari la shule.
11. Atashughulikia usafiri wa wanafunzi.
12. Atapanga ratiba ya walimu wa zamu.
13. Atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Malezi na Utamaduni.
14. Atafanya kazi nyingine zozote ambazo atapewa na Mwalimu Mkuu.
Leave a Comment