Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the post-views-counter domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /www/wwwroot/net.wazaelimu.com/wp-includes/functions.php on line 6131
Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) 2025

Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) 2025

Orodha ya Majina ya Walioitwa Usaili Uboreshaji wa daftari la Mpiga kura 2025: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Katiba hiyo, Ibara ya 65, inaelekeza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani ufanyike kila baada ya kipindi cha miaka mitano (5).

Tanzania inatumia mfumo wa uchaguzi ambao mgombea mwenye kura nyingi kuliko mgombea mwingine hutangazwa kuwa mshindi (First Past The Post). Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 41 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, Kifungu cha 35F(8) na Kifungu cha 81 (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi, Waandishi Wasaidizi, na ”BVR Kit Operators”. Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura pia wanashirikishwa.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 15A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Kifungu cha 17A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura. Mawakala hawa wanawajibika kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia sheria, kanuni, na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

DOWNLOAD PDF BELOW

MOROGORO

Jimbo la Ulanga

Leave a Comment